Kuhusu Sisi

Karibu sana

Kuhusu Sisi

Tajiri Ng’ombe Enterprises ni jina rasmi la biashara la Dan’G Group of Companies Limited, yenye makao makuu Mjini Dodoma, Tanzania. Tumejikita katika biashara ya mifugo kupitia mnyororo mzima wa thamani, kwa lengo la kutoa suluhu bunifu na endelevu kwa changamoto zinazowakabili wakulima na wanunuzi wa ndani na nje ya nchi.

Dhamira Yetu

Kuwa daraja la kuaminika kati ya wakulima wadogo na masoko yenye tija, tukihakikisha pande zote mbili — mkulima na mnunuzi — wananufaika kupitia biashara yenye uadilifu, ubora, usambazaji thabiti wa nyama, na miundombinu salama ya kuuza ndani na nje ya nchi.

Maono Yetu

  • Kuchangia kuunda sekta ya kisasa ya mifugo nchini Tanzania, ambapo:
  • Wakulima wanajengewa uwezo na kuimarishwa kiuchumi,
  • Wanunuzi wanapata mifugo na bidhaa zake zenye ubora wa juu,
  • Mnyororo mzima wa thamani unachangia moja kwa moja katika usalama wa chakula, ukuaji endelevu wa uchumi wa taifa, na ushindani wa kimataifa kupitia export.

Tunachanganya maarifa ya kitamaduni ya ufugaji na teknolojia za kisasa ili kuimarisha ufanisi wa usimamizi, kuboresha huduma za mifugo, na kuunganisha wakulima na masoko yenye uhakika. Kwa njia hii, tunahakikisha thamani inaongezwa katika kila hatua ya mnyororo wa mifugo — kuanzia shambani hadi sokoni na hata kimataifa.

Kwanini Utuchague

Ununuzi wa ng’ombe,

Unenepeshaji wa ng’ombe na huduma za mifugo,

Usafirishaji wa kisasa na salama,

Usambazaji wa nyama bora nchini,

Uuzaji wa mifugo na bidhaa zake nje ya nchi

Scroll to Top